Afisa wa kandanda wa Marekani Chuck Blazer amefariki akiwa na unmri wa miaka 72.
Blazer ambaye alipigwa marufuku ya maisha kutoka shughuli za kandanda mwaka 015 amefariki kutokana na ugonjwa wa saratani.
Mwaka 2013 alikiri kuhusika kwenye ufisadi, ulanguzi wa pesa na kukwepa kodi lakini akakubali kusaidia uchunguzi kufichua ufisadi katika shirikisho la Fifa.
Taarifa zake zisababisha kuwepo mashtaka dhidi ya maafisa 14 wa zamani na wa sasa wa Fifa na kuchangia kuondolewa kwa Sepp Blatter ambaye alikuwa ni Rais wa Fifa.
Alihudumu kama afisa wa kamati kuu wa Fifa kutoka mwaka 1997 na 2013 na wakati wa kipindi alipokea mamilioni ya pesa kwa maisha yake ya anasa.
Mwaka 2013 ripoti ya kamati ya Concacaf, Shirikisho la kandada la kaskazini na kati kati mwa Amerika ilisema kuwa alipokea dola milioni 20.6 kama marupurupu kati ya mwaka 1996 na 2011.
Post a Comment