Mwaandishi wetu
TIMU ya Soka ya Makambako worries,ya Iringa imeifunga bao 7 bila Timu ya Silabu Fc ya Masasi Mkoani Mtwara katika mchezo wa ligi daraja la pili inayokutanisha mabingwa wa mikoa kituo cha Lindi.
Makambako worries walianza kuandika kalamu ya magoli dakika 6 kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Edward Magani, Kukiwa kumebaki dakika moja kuwa mapumziko, makamabako walipata goli la 4.
Kipindi cha pili timu ya Silabu Iliingia uwanjani ikiwa na nguvu mpya baada ya kupata mawaidha kutoka kwa walimu wao,ambapo katika dakika ya 31 ilipata kona isiyo na matunda
Kona hiyo iliongeza mori ya mchezo kwa vijana wa Makambako ,kwani katika dakika ya 32 aliipatia bao la 5 na dakika 38 bao la 6, na dakika 56 bao la 7 na la mwisho kwa upande wao.
Hadi mwisho wa mchezo Makambako worries wakatoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 7 bila dhidi ya Silabu Fc ya Masasi mkoani Mtwara
Post a Comment