Tanzania imepoteza
takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola milioni 84 za
Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017
kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi March mwaka huu na Rais John Magufuli.
Ripoti
hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya kwanza iliyojikita kueleza
kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na
usafirishaji wa mchanga wenye madini.
Kamati
hii ya sasa iliundwa na wataalam wa masuala ya uchumi na wanasheria
ambao walikuwa na jukumu la kutazama mikataba ya madini na athari za
kiuchumi kwa Tanzania.
Katika Ripoti ya Jumatatu, Tume imedai kuwa
Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada, Acacia ambayo ni
kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini humo, hivyo
imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni
kutoka Ikulu, Rais Magufuli amemtaka waziri wa sheria Profesa
Paramagamba Kabudi kupitia mikataba yote ya madini.
Ameahidi kutekeleza mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati.
Ripoti iliopita ilisababisha Waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo kusimamishwa kazi.
Post a Comment