0

Na. Ahmad Mmow, Dar es Salaam.
Imeelezwa kwamba jumla ya wananchi 1522 wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru mkoani humu walijitokeza kwa hiari kupima Virusi Vya UKIMWI. Hayo yameelezwa leo na mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alipokuwa anakabidhi mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam, Paul Makonda katika viwanja vya Kongowe.
Zambi ambae mkoa wake ulipokea mwenge huo tarehe 21 mwezi huu nakukimbizwa katika halmashauri zote za mkoa huo kwa umbali wenye urefu wa kilometa 1202, alisema katika kipindi ambacho mwenge ulikuwa mkoani humo watu 1522 walijitokeza kwa hiari kupima maambukizi ya VVU. Zambi ambae katika mkoa wake, mwenge huo ulitembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo 51 yenye thamani ya shilingi 11.24 bilioni, alisema kujitokeza huko kulitokana na uhamasishaji uliofanyika katika kipindi chote ambacho ulikuwepo mkoani humo.
Mkuu huyo wa mkoa aliyataja matokeo ya upimaji huo kuwa watu 20 ambao ni sawa na 1.3% walibaini kuwa na maambukizi. “Lakini pia upimaji wa malaria ulifanyika waambukizwa na VVU Wazingatie ushauri na masharti waliyopewa wakati wanafanya upimaji”. Huku akitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa hiari kupima afya zao.
Aidha Zambi alisema katika mkoa huo vita dhidi ya dawa za kulevya inapiganwa kwa juhudi kubwa na maarifa. Ambapo mafanikio hayo yamekuwa na matokeo chanya kwa kukamatwa kilo 1,790 na gramu 582 za dawa za kulevya. “Mchanganuo wa dawa hizo za kulevya ni heroini gramu 177.94 na bangi yenye uzito wa kilo 1,790 na gramu 405. Ambapo watuhumiwa 256 wamefikishwa mahakamani,” alisema Zambi.
Mwenge huo katika mkoa Dar-es-Salaam unatarajiwa kukimbizwa kwa umbali wenye urefu wa kilometa 1594. Utambelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo 40 yenye thamani ya shilingi 242.36 bilioni
.

Post a Comment

 
Top