Mkuu wa wilaya ya
Liwale,mhe. Sarah Chiwamba wa pili kutoka kushoto akimpatia mototo chanjo
(picha na Mwandae Mchungulike).
Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Liwale,Mary Ding'ohi akitoa neno katika uzinduzi wa chanjo leo aprili 24
Na Mwandae Mchungulike,Liwale
Mkuu
wa wilaya ya Liwale Mheshimiwa Sarah Chiwamba amewahimiza wananchi wa Wilaya ya
Liwale kutowaficha watoto wao na badala yake wawapeleke kwenye vituo vya afya
kwa ajili ya kupata chanjo.
Mheshimiwa
Chiwamba ameyasema hayo leo Aprili 24 alipokuwa akizindua amezindua siku ya
chanjo kwa watoto katika hospitali ya wilaya Liwale.
“Ndugu
zangu tubadilike na tuachane nay ale mazoea ya kutowapeleka watoto wetu
hospitali kwa ajili ya chanjo. Hizi chanjo ni muhimu sana kwa ajili ya kuzuia
magonjwa ya aina mbalimbali kwa watoto wachanga” Alisema mheshimiwa Chiwamba.
Akizungumza
kwa niaba ya akina mama waliohudhuria kwenye zoezi hilo, Bi. Doto Alawi amesema
jamii inatakiwa kutambua na kuthamini umuhimu wa chanjo kwa watoto kwani
inamkinga mtoto dhidi ya magonjwa yanayokingika. Pia aliwahamasisha akina mama
wengine kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya kupatiwa chanjo.
Zoezi
hilo la chanjo limeanza Aprili 24 na litaendelea hadi Aprili 30 mwaka huu na
likiwa limebeba kauli mbiu isemayo “Jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya”
Post a Comment