Baba
mmoja aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Mademba (39) mkaazi wa
Kianga atiwa mikononi mwa polisi kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa
kambo mwenye umri wa miaka 13.
Taariza
zilizothibitishwa na kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi Kamishna
msaidizi muandamizi wa Polisi Hassan Nassiri Ali amesema tukio hilo la
kusikitisha baina ya mwezi machi na april 19 mwaka huu huko kianga
wilaya ya magharibi A.
Aidha
kamanda hassan amesikitishwa sana na tukio hilo na kuiomba jamii
kurudi katika maadili mema kwani ni jambo la ajabu sana kusikia mwana
familia kufanya tukio la kinyama katika familia yake.
Hata
hivyo amesema Mtuhumiwa wa tukio hilo ameshakamatwa na polisi na baada
ya upelelezi kukamilika atapelekwa mahakamni kujibu shtaka lake

Post a Comment