Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi pamoja na makamu wa Rais Mstaafu
Dr.mohamed Gharib Bilal wametoa wito kw wahitimu wa Chuo Kikuu Cha
kiislam cha Al-Azhar cha Misri waliopo nchini kuwa chachu ya mabadiliko
ya vijana katika nyanja ya Elimu ya dini, Uchumi pamoja na kubuni mbinu
zitakazowawezesha vijana kutumia elimu wanayopata kujikwamua kiuchumi.
Aidha wamewataka wasomi hao wenye Shahada za Elimu ya Dini ya kiislam, kubuni mikakati katika kutoa elimu sahihi katika kupambana na mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa katika kipindi hiki cha utandawazi kupitia mitandao ya Kijamii.
Vingozi hao wastaafu wametoa wito huo wakati wa hafla fupi ya umoja huo kukabidhi vyeti wahitimu zaidi ya 80 waliosoma nchini Misri, pamoja na kuadhimisha hafla ya Maulid ya mtume iliyofanyika katika kituo cha Kiislam cha Markaz chang’ombe jijini dsm.
Awali Rais wa Umoja wa wahitimu hao Yaqub Mrisho alisema Umoja huo unadhamiria kujenga shule na vyuo vya kufundishia elimu ya dini ya kiislam, lakini pia elimu ya uchumi na ujasiliamali.

Post a Comment