0


Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashitaka matatu yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.
                 
   Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dwa za kulevya aina ya bangi. 

Wakili Katuga amesema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Wema Sepetu mnamo tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio watuhumiwa watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.

Msanii huyo na wenzake wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na wadhamini wawili na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 22 mwaka huu itakapotajwa tena na kwamba bado uchunguzi unaendelea

Post a Comment

 
Top