WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Waziri
Mkuu amesema Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo
amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio na kwa manufaa
ya Taifa.
Pia
amewataka ATCL kuacha kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa
mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa
mapato hayo.
Katika
hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika
eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.
Hata hivyo
Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba
ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
Post a Comment