Jeshi la Polisi Mkoa wa
kusini Unguja linawashikilia vijana wawili wakazi wa
Makunduchi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14
Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa kituo
cha Polisi Makunduchi, wilaya ya kusini Ispecta Khamis Ali Omar amewataja
watuhumiwa hao kuwa ni Ali Khatib 53 na Ramadhan Issa Simai 45 ambapo Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguza wa tuhuma hizo
Kwaupande wake mzazi wa mtoto huyo amesema walimpeleka mtoto huyo hospitali kwa ajili ya vipimo na kubainika kufanyiwa kitendo hicho
Hata hivyo mwanaharakati wa maswala ya wanawake na watoto wa Makunduchi Bi
Subira Ame Msondo amesema bado jamii haina muamko wa kuripoti kesi hizo na
kutaka elimu kuendelea kutolewa ili kuvitokomeza vitendo hivyo.
Post a Comment