Nchi za ukanda wa
kusini magharibi mwa bahari ya hindi zimetakiwa kuandaa sheria zitakazokuwa na
uwiano katika nchi wanachama ili uvuvi katika bahari kuu kuwa wa mafanikio
Akizungumza
kwa niaba ya waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Visiwani Zanzibar, Mh Hamad Rashid, Naibu
katibu mkuu anaeshuhulikia mifugo na uvuvi Dk Islam Salum Seif amesema uwiano
huo wa sheria unapaswa kujadiliwa kwakina na nchi wanachama ili kuwa na uvuvi
wenye tija.
Nae mkurugenzi mkuu wa
mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu Tanzania Hosea Mbilinyi amezitaja changamoto
zinazozikabili nchi wanachama ni pamoja na viwango tofauti vya leseni miongoni
mwa nchi wanachama hatua inayotoa mwanya kwa wamiliki wa meli za uvuvi kutoka
nje kuchagua nchi ya kwenda kwa lengo la kufuata kiwango cha chini cha leseni.
Mkutano
huo wa siku tatu wa wadau wa uvuvi wa bahari kuu kutoka nchi wanachama, ukanda
wa kusini magharibi mwa bahari ya hindi unafanyika katika hoteli ya Marumaru
mjini Unguja.
Nchi wanachama ni
pamoja na Tanzania, Kenya, Somalia Comoro, Msumbiji, Yemen na jamhuri ya Afrika
ya kati.
Post a Comment