WAZIRI
wa elimu na mafunzo ya amali Visiwani Zanzibar Mh Riziki Pembe Juma amewataka
walimu na kamati ya wazazi ya Shule ya Sekondari Lumumba kuongeza juhudi ili
kuendelea kutoa wanafunzi bora kila mwaka.
Shule
hiyo ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi Visiwani Zanzibar katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2016, ambapo kati ya wanafunzi 106 waliofanya
mtihani huo, 54 wamefaulu katika daraja la kwanza, 42 katika daraja la pili na
wanafunzi 10 daraja la tatu.
Akizungumza
na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Lumumba alipotembelea Shule hiyo,
Mhe. Riziki ameshauri kutumika mbinu mbadala kuhakikisha shule hiyo inapata mafanikio
zaidi huku akiahidi wizara yake kutoa ushirikiano wa hali na mali.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo, Mussa Hassan ameahidi kuweka mikakati maalumu kuhakikisha
skuli hiyo inafaulisha zaidi katika mitihani ya mwaka huu huku akiwasisitiza
wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuitangaza shule hiyo kitaifa na kimataifa.
Post a Comment