Kamanda wa polisi mkoa
wa mjini magharib Visiwani Zanzibar Hassan Nassir amewataka madereva kuacha kukimbia baada ya
kutokea kwa ajali na badala yake wanapaswa kuripoti katika kituo cha polisi.
Ametoa
wito huo kutokana na siku za kuongezeka kwa tabia ya baadhi ya madereva
kukimbia pindi wanapohusika katika ajali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Amefafanua kuwa dereva
anaehusika katika ajali anapaswa kufika katika kituo cha polisi ndani ya saa
24.
Ameongeza
kuwa dereva anaeamua kukimbia baada ya ajali, akikamatwa mbali na kesi ya ajali
pia huadhibia kwa kosa la kukimbia.
Katika
juma lililopita zimeripotiwa ajali 7 za barabarani katika mkoa wa mjini
magharibi.
Post a Comment