Mamlaka nchini
Tanzania imewataka watu watatu inaowashutumu kwa kuwa wapenzi wa jinsia
moja kuripoti kwa maafisa wa polisi ili kuhojiwa la sivyo wakamatwe.
Naibu
waziri wa afya nchini humo Hamis Kingwangalae amesema kuwa watatu hao
walikuwa wakisambaza harakati za wapenzi wa jinsia moja kupitia mitandao
ya kijamii kinyume na sheria.
Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja
ni kinyume na sheria nchini Tanzania na walio na hatia hupewa adhabu ya
kifungo cha hadi miaka 30 jela .
Mwaka uliopita ,waziri wa afya
alitangaza kwamba mpango wa kuwapatia matibabu wapenzi wa jinsia moja
walio na virusi vya HIV utasimamishwa.
Serikali pia imetishia kupiga marufuku makundi ambayo yanaunga mkono haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja.BBC
Post a Comment