0
Wakati chama cha mapinduzi ccm kinajiandaa na  uchaguzi wa ndani, wanachama wa chama hicho Zanzibar wametakiwa kuchagua viongozi kwa kuzingatia sifa na uadilifu wao ndani ya chama.
            
     

        Mjumbe wa kamati ya siasa mkoa ambae pia ni mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Muhammed ametoa rai hiyo alipokuwa akifungua kikao cha jumuiya ya wazazi wilaya ya dimani kilichofanyika katika tawi la ccm kiembe samaki.

Amesema katika kufanikisha azma ya kuwa na ccm mpya na tanzania mpya viongozi pamoja na wanachama wanapaswa kuibua mikakati mipya ya kuwabaini pamoja na kuondoa viongozi wasiokuwa waadilifu.

Akiwasilisha mada ya uchaguzi, katibu wa ccm wilaya ya kati ali yussuf amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali ili kuweza kukitumikia chama hicho kikongwe zaidi hapa nchini.

Post a Comment

 
Top