Taasisi za umma na za
binafsi Visiwani Zanzibar zimetakiwa kuendesha mafunzo kupambana na vitendo vya rushwa katika
taasisi zao ili kukabiliana na vitendo hivyo Zanzibar.
Afisa uhusiano mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar
ZAECA Mwanaidi Suleiman amesema kuendelea kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika
taasisi hizo kunatokana na wafanyakazi katika taasisi hizo kukosa taaluma ya vitendo
hivyo.
Ameongeza kuwa takwimu zinaonesha asilimia ya vitendo vya
rushwa kwa upande wa Zanzibar ipo chini hivyo ZAECA wanaangalia namna ya
kuondoa kabisa vitendo hivyo.
Aidha afisa huyo ametoa rai kwa jamii kuacha muhali juu ya
vitendo vya rushwa na badala yake kuripoti vitendo hivyo katika mamlaka
zinazohusika ili wachukuliwe hatua husika.
Post a Comment