0


Wanachama wa chama cha mapinduzi Zanzibar wameshauriwa kufuata nyayo za waasisi wa chama hicho kwa kujitolea na kuweka mbele dhana ya uzalendo katika kujenga miundombinu ya kudumu itakayowasaidia  vizazi vya sasa na vijavyo.
                       


Ushauri huo umetolewa na naibu katibu mkuu wa ccm Zanzibar, vuai ali vuai wakati akifungua kongamano la ccm wilaya ya kati unguja, amesema maendeleo yaliyopatikana ndani ya serikali na chama yametokana na juhudi kubwa zilizofanywa na wazee wa chama hicho.

MH: Vuai amewataka wafuasi wa ccm kila mmoja kwa nafasi yake kufanya jambo la maendeleo litakalobaki katika vitabu na historia ya kumbukumbu za chama ili vizazi vijavyo virithi taasisi yenye nguvu katika suala la maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Mh:Vuai amefahamisha kuwa waasisi hao wameacha miundombinu na vitega uchumi mbali mbali katika sekta mbali mbali zikiwemo afya, elimu na majumba ya maendeleo yaliyopo kila mikoa nchini ambayo ni matunda ya waasisi wa muungano na mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Akizungumzia miaka 40 ya kuzaliwa kwa chama hicho amesema wananchi wa mijini na vijijini wameweza kunufaika na fursa mbali mbali zinazotokana na sera za chama hicho.

Sambamba na hayo amewapongeza rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dkt. ali mohamed shein pamoja na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania dkt. john pembe magufuli kwa juhudi zao za kusimamia kwa uadilifu fursa za kimaendeleo kwa maslahi ya nchi.

Mh: naibu katibu mkuu wa ccm Zanzibar anafanya ziara maalum kunzia ngazi za mashina hadi wilaya kwa lengo la kukagua hali ya kisiasa na kuratibu changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo mbali mbali  ili zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu kupitia mamlaka husika.

Post a Comment

 
Top