Jeshi
la polisi Visiwani Zanzibar limewaachia kwa dhamana watu sita wanaotuhumiwa kwa utumiaji wa dawa za kulevya aina ya
shisha.
Akizungumza
na waandishi wa habari kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Mjini Magharibi hassani nasir amesema jeshi la polisi kwa
sasa linaendelea na uchunguzi na kuhakikisha wanatokomeza tatizo la uvutaji shisha katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
katika hatua nyengine kamanda Nassir amewataka vijana kuacha kuacha kujiingiza katika magenge yasiofaa ikiwemo
uvutaji wa shisha na badala yake, watumie muda huo kufanya shughuli za
kimaendeleo
vita
hiyo ya kukabiliana na matumizi ya shisha ndani ya mkoa wa mjini imezidi
kushika kasi baada ya mkuu wa mkoa wa mjini magharib Ayoub Moh’d siku chache
zilizopita kupiga marufuku utumiaji wa shisha katika mkoa wake.
Post a Comment