Katika kuelekea
maadhimisho ya siku ya sheria Zanzibar wananchi wametakiwa kutii sheria bila ya
shuruti ili kuepusha kukwazana na serikali kwa kuvunja sheria.
Wito huo umetolewa na
Kamanda wa Jeshi la polisi wa mkoa wa mjini magharibi Hassani Nassir alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake madema mjini Unguja .
Kamanda Nasir amesema
lengo la kuadhimisha siku ya sheria Zanzibar
ni kuwapa elimu wananchi juu kufanya vitendo kwa kufata sheria ya nchi .
Aidha amewahakikishia wananchi na jamii kwa ujumla
kutunza usalama wa raia na mali zao siku ya maadhimisho tarehe 9 mwezi 2 mwaka
huu .
Hata hivyo amewataka
wananchi kujishughulisha na harakati zao za maisha kwa kuzingatia sheria na
yoyote atakae bainika kwenda kinyume na sheria ya nchi hatua kali za kisheria
zitachukuliwa.
Kauli mbiu ya siku ya
sheria ya mwaka huu ni simamia sheria na maadili katika utendaji haki.

Post a Comment