Vijana wanaoishi Visiwani Zanzibar wameshauriwa kutumia mfumo mpya wa
kuomba ajira kupitia mfumo wa kielektroniki ili kuepuka usumbufu wanapotumia njia ya kawaida.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini
ofisi ya rais sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma
Zanzibar, Riziki Abrahaman
alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa chuo
kikuu cha SUMAITI Chukwani wilaya ya magharibi B Unguja.
Amesema serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia sekreterieti ya ajira katika utumishi
wa umma imeanzisha mfumo mpya wa kuomba ajira kupitia mtandao wa e-aplication
ili kuwarahisisha waombaji wa ajira kuweza kutuma maombi yao kwa haraka na bila
ya usumbufu.
Ameongeza kuwa mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa
kuondosha kadhia kadhaa katika
mchakato wa kuajiri watu kama vile rushwa
na upotevu wa nyaraka muhimu za waombaji vikiwemo vyeti vya kuzaliwa,
kumaliza skuli na vyuo.
Aidha ameawataka wanafunzi na wananchi wa Zan zibar
kutumia fursa waliyonayo kisheria ya kuomba ajira zinazotolewa na
Serikali ya jamuhuri ya
muungano
wa Tanzania katika taasisi
mbali mbali ili kunufaika na
haki zao kikatiba.

Post a Comment