0


Ofisi  ya mufti Zanzibar imemsimamisha ustadhi Hakim Mbarouk Hamadi wa Madrasatul Ghinayatuli Qurani kujihusisha na masuala ya kufundisha kufuatia kitendo cha kuwadhalilisha kwa kuwaadhibu kupita kiasi wanafunzi 11 wa madrasa yake.
                 
      Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga



Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na katibu wa mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga imeeleza Hatua hiyo imekuja baada ya mazungumzo na mtuhumiwa huyo yaliyofanyika katika kituo cha polisi cha bububu wilaya ya Magharib A unguja ambapo mwalimu huyo anashikiliwa.
Mwalimu huyo anatuhumiwa kuwapiga wanafunzi kwa viboko kisha kuwavua nguo
katia hatua nyengine Shehe Soraga amesema mwalimu huyo amekiri kufanya kitendo hicho lakini si kwa kiwango kinachozungumzwa.
Pamoja na hayo Afisi ya mufti Zanzibar imelaani vikali kitendo cha mwalimu huyo wa madrasa na kuwataka walimu wengine wa madrasa zote za unguja na pemba waache vitendo vyote vya unyanyasaji na udhalilishaji kwa watoto vikiwemo ulawiti ,upigaji bakora kupita kiasi pamoja na ubakaji.
        Katika hatua nyengine Jumuiya ya maimamu Zanzibar JUMAZA na wao wamelaani tukio hilo ambapo Naibu mtendaji wa jumuiya hiyo Khamis Yussufu kulinagana na mafundisho ya dini ya kiislamu, kuwanasihi watoto kuipenda na kuielewa dini yao.

Post a Comment

 
Top