Masheha wa Shehia mbali mbali Zanzibar wametakiwa
kufatilia na kupambana na matumizi ya misumeno ya moto ambayo imepigwa marufuku
na serikali.
Hayo
yamesemwa na katibu mkuu wa wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi Ali Juma
Ali alipokuwa akizungumza na wadau mbali mbali wakiwemo masheha na wakuu wa
wilaya amesema misumeno ya moto kwa Sasa imepigwa marufuku na haitakiwi
kutumika kwa sababu imebainika kuathiri vibaya mazingira.
Hata
hivyo amesema serikali inawakumbusha watendaji wa shehia wakiwemo masheha na
wakuu wa wilaya kwamba misumeno hiyo haitakiwi kutumika kwa ajili ya ukataji wa
miti ikiwemo minazi na miti mengine.
Nao
baadhi ya wamiliki wa ekari tatu zilizotolewa na serikali kwa ajili ya matumizi
ya kilimo akiwemo Ali Hilka mkaazi wa kitumba na Issa Uledi mkaazi wa chuini
wilaya ya kati wamelalamika kuvamiwa mashamba yao usiku na kukatiwa minazi saba.
Nae
mkuu wa wilaya ya kati Mashavu Sukwa amesema wameanza kuchukua hatua kali kwa
watu waliouza ekari tatu ambapo baadhi ya wakulima wamenyanganywa na kurudishwa
serikalini.
Post a Comment