Mwanafunzi wa Iran Benham Prtopour baada ya kuruhusiwa na idara ya uhamiaji nchini Marekani kuelekea Boston
Jaji mmoja wa
Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump
ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya
Kiislamu kuingia nchini Marekani.
Jaji wa Seattle alipuuzilia
mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri
hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea
kusikilizwa mahakamani.
Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.
- Trump kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani
- Donald Trump kuwarejesha wahamiaji kwao
- Jaji apiga marufuku amri ya Trump kurudisha wahamiaji makwao
- Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
- EU: Donald Trump ni tishio kwa Ulaya
- Trump: Mexico watalipia ukuta '100%'
Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa
zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi
ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.
Wakati
huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema
kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika
tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran
katika paspoti yake.
Post a Comment