Mwanamke akatwa masiko yake na mumewe
Mwanamke mmoja wa
miaka 23 kutoka nchini Afghanistan ameielezea BBC kwamba mumewe
alimfunga kamba na kumkata masikio yote mawili katika mzozo wa
kinyumbani katika mkoa wa kaskazini wa Balkh.
Mwanamke huyo Zarina kwa sasa yuko katika hali nzuri hospitalini.
''Sijatenda dhambi lolote'' ,alisema.''sijui kwa nini mume wangu alinifanyia hivi''.
Mume huyo kwa sasa ameenda mafichoni katika Ulaya ya kashinda kufuatia shambulio hilo kulingana na maafisa wa polisi.
Zarina
ameambia chombo cha habari cha Pajhwok kwamba shambulio hilo ambalo
anasema halikusababishwa na hatua yoyote lilifanyika baada ya mumewe
kuamka.
Mwanamke huyo aliolewa akiwa na umri wa miaka 13 na ameiambia BBC kwamba uhusiano wake na mumewe haukuwa mzuri.
Zarina alilalamika kwamba mumewe alijaribu kumzuia kutowatembelea wazazi wake, amesema hataki kuwa naye tena.
"Ananishuku sana na kila mara unituhumu kwa kuzungumza na wanaume wengine wakati ninapoenda kutembelea wazazi wangu'' ,alisema.
Ametaka akamatwe na kushtakiwa.
Post a Comment