Kampuni ya ndege ya Qatar Airline
Idara ya forodha ya
Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda
ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais
Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi,
wakataliwe kuingia Marekani.
Shirika la ndege la Ghuba, Qatar Airways, lilisema litaanza kupakia abiria haraka.
Hatua hiyo inafuata saa tu baada ya jaji wa mahakama ya taifa ya Marekani, kuzuia amri hiyo ya Rais Trump kwa muda.
Mahakama iliamua kuwa hatua ya rais ilivunja katiba, ambayo inakataza dini moja kupendelewa kushinda nyengine.
Serikali inasema itakata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Katika hotuba yake ya kila juma, rais alisema amri yake ilikusudiwa kuwalinda Wamarekani
Post a Comment