Manchester United waliilaza Souythampton mabao 2-1 ili kushinda kombe la EFL
Mshambuliaji wa
Manchesater United Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la ushindi dakika za
mwisho na kumpatia mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho kombe
lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo kwa kuishinda Southampton.
Southampton
walionyesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo lakini wakavunjwa moyo
na uamuzi wa utata uliompa bao la ushindi raia huyo wa Sweden mwenye
umri wa miaka 35. Wachezaji wa Southampton wakisherehekea bao la Manolo Gabbiadiani
Mshambuliaji wa Saints Manolo Gabbiadiani alifunga
bao lililokataliwa kabla ya Manchester United kupata bao la pili
kupitia Ibrahimovic kunako dakika 19 kabla ya Jesse Lingard kufunga
ikiwa imesalia dakika saba mechi kukamilika.
Southampton ilifunga mabao yake mawili kupitia Gabbiadiani katika vipindi vyote viwili vya mechi. Zlatan Ibrahimovic
Oriel Romeu alipiga mwamba wa goli kabla ya
Ibrahimovic kufunga kupitia krosi iliopigwa na Anders Herrea dakika tatu
kabla ya mechi kukamilika na hivyobasi kuipatia ushindi Manchester
United.
Post a Comment