
Mwaandishi wetu
IMEBAINIKA baadhi ya madereva wa Pikipiki au maarufu boda
boda mkoani Lindi wamekuwa wanawaweka wanafunzi shule za msingi na
sekondary ujauzito wakati wakiwa bado shuleni mwaka jana.
Hayo yaliyobainishwa na mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi
wakati alipokuwa akizungumza na wananchi, viongozi wa ngazi ya wilaya serikali
ya kijiji pamoja na kata ya Litingi, wilayani humo, alisema kwamba moja ya
wilaya kuna wanafunzi wa sekondary saba walipatiwa ujauzito na madereva hao,
mwaka jana.
Tatizo linalowakuta wanafunzi hao kuomba lifti kwenda
shuleni hapo ni moja ya chanzo cha kupatiwa ujauzito wanafunzi wanaosoma mbali
na shule zao kutoka nyumbani kwenda shuleni.
Aliongeza kwa kusema kwamba wazazi toeni nauli kuwapa
wanafunzi siyo mnaawaacha wapewe lifti, ni hatari kwa vijana hao.
Aidha aliwataka viongozi wa serikali za vijiji hadi wilaya
kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanawaweka wanafunzi mimba.
'Hivi karibuni kuna mzee mmoja alimweka mimba mwanafunzi
sasa yuko ndani anatumikia kifungo.
'Mimi nasema nataka hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi
yao siyo kuwaachia wazazi na wati mimba kudanganyana'' alisema Zambi.
Alisema kwamba kaaeni macho na umakini hasa hawa wanafunzi
wa kike hizi lifti wanazozitaka ni changamoto ni lazima wazazi mjitoe
kuwasaidia wakiwa bado mashuleni.
Aidha
aliwashari wazazi kutoa michango ya shuleni hasa kwenye ujezni wa vyoo ili
kusaidia wanafunzi pamoja na walimu kukaa maeneo yenye usalama kiafya
Post a Comment