
Mwandishi wetu
Watu 1,200 mjini Lindi
mkoani humo wanatarajiwa kufikishwa Mahakama ya mwanzo kutokana kutuhumiwa
kutojenga vyoo katika majumbani mwao wanakoishi,
Hayo yaliyobainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Lindi Joumary Satura leo wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa yake
mbele ya ya wajumbe wa baraza la madiwani kwenye kikao cha baraza la madiwani
cha nusu ya mwaka 2016/2017 mjini hapa.
Alisema kwamba mamlaka iliamuwa kuchukuwa hatua hiyo baada
ya kujiridhisha kaya hizo wanaishi bila ya kuwa na vyoo na kusababisha
hatarishi kutokea magonjwa ya milupuko ya kuhara na matumbo.
Satura alisema kwamba elimu zinapitishwa mara kwa mara juu
ya umuhimu wa kuwa na vyoo, lakini jamii nayo inakuwa na wakati mgumu
kutekeleza elimu hiyo.
'Tumeamuwa kuchukuwa hatua hiyo ili kuweza kukomesha kwa
wananchi wengine ambao hawana na vyoo kuweza kujenga'alisema mkurugenzi huyo.
Aliongeza kwa kusema kwamba jamii inapaswa kutiaa sheria
zinazowekwa na mamlaka husika na kuzitekeleza kwa wakati unaotakiwa.
Aidha alisema kwamba barua za kuitwa zilishaanza kutolewa
juu ya watuhumiwa hao kwenda mahakamani.
Alisema kwamba ufuatiliaji unandelea ili kuweza kubaini kaya
nyingine ambazo hazina vyoo.
Hivi karibuni Serikali ya mkoaa wa Lindi ilishwai kusema
kwamba wilaya za Kilwa na Liwale zinaongoza kwa wananchi wake kutkuwa na vyoo
mkoani humo.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi aliyasema hayo katilka
kijiji cha Tingi wilayani Kilwa.
Alisema kwamba kwa hiyo wananchi wajenge vyoo na
ikiwezeka mpaka mashuleni kama hakuna huduma hiyo wachangie
Post a Comment