Imeeelzwa kuwa
kama yasingefanyika Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12 Mwaka 1964 himaya ya
Sultan wa Oman ilioweka makaazi yake tokea mwaka 1832 ingeendelea
kuvikalia visiwa vya Unguja na Pemba kwa kuitumia hati ghiliba ya uhuru
bandia uliotolewa na Waingereza Mwaka 1963.
Mwonekano
wa visiwa vya zanzibar
Waziri wa zamani wa
SMZ aliyekuwa na dhamana ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Vikosi vya SMZ Mzee
Ali Haji Ali amebainisha hayo katika mshijiano maalum yaliofanyika
nyumbani kwake Mwanakwerekwe wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani hapa.
Mzee Ali alisema
vijana 14 wa ASP walioshiriki kufanya Mapinduzi ya zanzibar kimsingi wamechukua
juhudi kubwa hadi kufanikiwa kuwakomboa waafrika wenzao wengi
walioteseka karne kwa karne na kudhulumiwa haki na utu wao.
Alisema wana
Mapinduzi hao 14 walioongozwa na Jemedari mkuu hayati sheikh Abeid Amani
Karume wataendelea kuhesabiwa kwa wema na kuthaminiwa kwa kiwango cha hali ya
juu kwa ushupavu na ujasiri wao .
Waziri huyo wa
zamani alisema baada ya kuona waafrika wamechachamaa kutaka uhuru wao na
kujitawala wenyewe, ulianzishwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1957 ambao hata
hivyo haukuweza kumpa nafasi sultan ya kubakia zanzibar kutokana na nguvu za
kisiasa za ASP.
Alieleza kuwa
chini ya vyama vingi chama cha ASP kiliungwa mkono na kukubalika mbele ya
waafrika huku kikieleza bayana msimamo wake kwamba iwapo ASP kitashinda
hakitakubali kumtambua sultan wa oman aliyehamia zanzibar.
Utawala wa
kimabavu chini ya uongozi wa sultani dhidi ya waafrika ulifikia kikomo tarehe
12 januari mwaka 1964 baada ya kufanyika mapinduzi Zanzibar.
Post a Comment