0

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema wizara yake haitowavumilia wale wote wanaojichukulia sheria mkononi hasa migogoro ya wakulima na wafugaji iliyojitokeza mkoani Morogoro huku akisema wizara hiyo itahakikisha inatoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Tindiga, Kilomo mkoani Morogoro. Amesema serikali yake haitavumilia uvunjifu wa amani unaosababishwa na watu wachache NA unaosababisha vifo, vilema wa kudumu na kuivuruga amani ya Morogoro, huku akisema kuwa hakuna mashamba wala mifugo ambavyo vinalinganishwa na uhai wa mtu.

Aidha Nchemba amewataka viongozi kuchukua hatua kali na mathubuti kwa wale wote watakaojihusisha na migogoro ikiwemo kujichukulia hatua mkononi ili kutenda haki kwa wananchi na kuwafanya waendelee kuwa na amani na vyombo vya maamuzi.

Kwa upande wa serikali mkoani Morogoro, kufuatia tukio la mkulima mmoja kuchomwa mkuki walimuomba waziri mkuu kuangalia upya uwezekano wa kufuta sheria inayowahusu wafugaji wa kimasai kutembea na silaha za kijadi na matokeao yake kutumika na kudhuru wengine.

Post a Comment

 
Top