0


 Simba SC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano  ya Mapinduzi  inayoondelea visiwani Zanzibar  baada ya hapo jana kushinda kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya KVZ ya Zanzibar

Shukrani  za dhati zimuendee mfungaji wa goli hilo Jamali Simba Mnyate bao ambalo limepatikana katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza
Bao hilo limepatikana baada ya mabeki wa kati wa KVZ kutega mtego wa kuotea ambapo Simba walifanikiwa kutegua mtego huo  na Jamal Simba Mnyate akafanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika  michuano hiyo tangu kuanza kwake mwaka huu.

Kabla ya hapo kulikuwa na mchezo wa awali uliopigwa  majira ya saa 10:30 za jioni  ikiwakutanisha Jang’ombe Boys  dhidi ya URA  na Jang’ombe Boys  ikafanikiwa kushinda mabao 2-1

Ushindi huo walioupata timu ya Jang’ombe  dhidi URA ni ushindi wa kwanza kwa vilabu vya Zanzibar kupata ushindi kwa vilabu kutoka nje ya Zanzibar vinavyoshiriki ligi ya mapinduzi yaliyozinduliwa rasmi tar  30 january 2016

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha point 6 huku  wakiwa  wamecheza michezo 2 na kulazimika kukaa kileleni mwa kundi A huku mabigwa watetezi  URA  wakiwa nafasi ya pili wakiwa wamecheza michezo miwili na kunyakua point 6

Post a Comment

 
Top