0



Dar  es Salaam Young African (wakimataifa) wamedhiirisha umahiri wa kilitandaza soka  katika michuano ya mapinduzi baada ya jioni ya leo  kupata usindi wa pili  mfululizo kwa kufanikiwa kuifunga Zimamoto bao 2 bila ya majibu mchezo ambao umepigwa majira ya saa 10:30 za jioni katika  uwanja wa Amani
Shukurani ziende kwa  mfungaji ya mabao hayo Saimon msuva  aliyefunga mabao hayo katika kipindi cha kwanza na kuifanya yanga ikienda mapumziko ikiwa inaongoza mabao 2-0 ambapo hadi dakika 90 zinamalizika hakukuwa na mabadiliko yeyote.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha point  6 na magoli  nane na kulazimika kuketi katika nafasi ya kwanza kwa msimamo wa kundi B,huku nafasi ya pili ikisalia kwa Azam wakiwa wamecheza mchezo mmoja na kufanikiwa kunyakua point 3 na goli 1
Dar  es Salaam Young African ilishuka dimbani kwa mara ya kwanza jumatatu ya tarehe 2-1-2017 na kufanikiwa kuwalaza kwa mabao 6-0 Jamhuri kutokea Kisiwani Pemba
Hata hivyo  mashindano hayo yataendelea majira ya saa 2:30 za usiku kwa kuwakutanisha Mabingwa wa Africa Mashariki na kati dhidi ya Timu ya Jamhuri kutokea kisiwani Pemba
Ikumbukwe Azam anaingia katika mchezo huo akiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda goli 1-0 katika mchezo wake cwa kwanza dhidi ya Zimamoto na Jamhuri nayo inashuka katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wao wa awali dhidi ya yanga baada ya kufungwa bao 6-0

Post a Comment

 
Top