Waziri mkuu Kassim majaliwa amefungua
kituo cha zima moto katika eneo la uwanja wa ndege wa karume, Magharibi Unguja
ikiwa ni muendelezo wa uzinduzi wa miradi mbalimbali katika shamrashamra za
miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kuzinduliwa kwa kituo hicho
itasaidia kuongeza usalama katika uwanja huo na kusisitiza kituo hicho
kinapaswa kuwa cha kwanza kutoa msaada endapo ikitokea hitilafu.
Pamoja na hayo Mhe. Majaliwa ametoa
pongezi kwa viongozi wa mamlaka ya uwanja huo wa ndege kutokana na utendaji wao
wa kazi huku akiwasisitiza kushirikiana katika kukitunza kituo hicho kipya kwa
maslahi ya umma .
Aidha waziri mkuu amewasihi wananchi
kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kushiriki kilele cha sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar katika kiwanja cha Aman mjini Unguja.
Post a Comment