Makamo wa rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania mh: Samia Suluhu Hassan amesema serikali ipo katika harakati ya
kurekebisha sheria ya ukazi ili kuwapatia fursa watanzania wanaoishi nje ya
nchi kumiliki ardhi pamoja na kuwa na makazi ya kudumu nchini.
Akiweka jiwe la msingi katika mradi wa
nyumba za makazi za ZSSF zilizopo Mbweni
nje kidogo ya mji wa unguja, amesema hatua hiyo itawasaidia watanzania
hao kuwa na uwezo wa kumiliki nyumba hizo.
Mama samia amesema kuja kuwekeza kwao
watanzania hao ni njia moja wapo ya kuyaenzi mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya
kuiunganisha jamii pamoja bila ubaguzi.
Kwa upande wake mkurugenzi mwezeshaji wa
mradi huo Abduliwakiri Hafidhi amesema
mradi huo unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka tatu ambapo mpaka sasa
tayari nyumba tano zipo katika hatua ya mwisho ambapo zitamalizika ifikapo
april mwaka huu.
Aidha amewasihi wananchi kujitokeza kwa
wingi katika kununua nyumba hizo huku ajira 80 zinatarajiwa kutolewa mara baada
ya kukamilika kwa ujenzi huo.
Post a Comment