WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka
kuwapeleka wakaguzi wa hesabu kwenda kukagua mapato na matumizi ya Mamlaka ya
Maji ya Mji wa Njombe (NJUWASA
Ametoa
agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye
viwanja vya shule ya Sekondari Mpechi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Waziri
Mkuu amesema wakaguzi hao mbali na kukagua mapato na matumizi ya mamlaka hiyo
pia waangalie kama wananchi walihusishwa katika ukokotoaji wa gharama za malipo
ya bili za maji.
Ametoa agizo hilo baada ya wananchi kuilalamikia mamlaka hiyo
kupitia mabango kwamba wanatozwa bili kubwa ya maji licha ya huduma hiyo
kupatikana kwa kusuasua katika mji huo.
Kufuatia malalamiko hayo Waziri Mkuu amemtaka Mkurugenzi
Mtendaji wa NJUWASA, Daudi Majani kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo ambapo amesema
kwa mwezi wanakusanya sh. milioni 75 zinazotumika kuendeshea na uboreshaji wa
huduma.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa
umma kujiwekea utaratibu wa kwenda kwa wananchi na kusikiliza changamoto
mbalimbali zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi badala ya kujifungia
maofisini.
Post a Comment