WAJUMBE wa kamati ya
Mawasiliano na Ujenzi ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, wametoa wiki moja kwa
mwakilishi wa Jimbo la Ole, Mhe. Mussa Ali Mussa, kuvunja sehemu ya nyumba yake
ambayo imekwamisha ujenzi wa barabara ya Ole-Kengeja.
Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Hamza Hassan Juma ambae pia ni Mbunge wa Kwamtipura, ameeleza
kusikitishwa na hatua ya mwakilishi huyo kushindwa kuvunja nyumba yake licha ya
kulipwa fidia tangu Novemba 2 mwaka jana.
Ameongeza
kuwa haipendezi kwa kiongozi kukwamisha kwa makusudi harakati za maendeleo
zilizopangwa na serikali kwa ajili ya wananchi.
Pamoja na hayo amemtaka
msimamizi wa mradi huo kuhakikisha wananchi waliobaki wanalipwa fidia na
kuhakikisha nyumba zilizothibitishwa zinavunjwa ili ujenzi wa barabara hiyo
kuwa wa uhakika.
Mradi wa barabara ya
Ole-Kengeja mpaka kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi
Bilioni 11.
Post a Comment