Wakati chama cha mapinduzi CCM kikiwa kwenye
shamrashamra za kuelekea miaka 40 tangu kuanzishwa kwake, katibu wa idara ya
itikadi na uenezi CCM Zanzibar BI WARIDE BAKARI JABU amesema maadhimisho hayo
yatafanyika katika ngazi za mikoa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar, Bi. Waride
amesema kila mkoa ulishaandaa ratiba za shughuli zitakazofanyika katika mikoa
yao pamoja na kuwepo kwa zoezi la usafi wa mazingira.
Amezitaja
shughuli nyengine kuwa ni kuwakagua wangonjwa na kuwafariji wazee wasiojiweza,
mikutano mikuu ngazi mbali mbali, zoezi
la kupanda miti katika maeneo mbali mbali ya kijamii na vyanzo vya maji pamoja
na michezo na makongamano
yatakayoeleza historia ya CCM na
mafanikio ya chama hicho katika kipindi cha miaka 40.
Pamoja
na hayo amesema chama cha mapinduzi
kinawashukuru kwa dhati kabisa wana CCM na wananchi wote wa jimbo la Dimani pamoja na kata za mikoa ya Tanzania bara iliyofanya
uchaguzi kwa kupiga kura kwa utulivu na kukipa chama hicho ushindi mkubwa.
Chama
cha mapinduzi kimezaliwa Februari 5 ya mwaka 1977 baada ya kuungana kwa chama
cha TANU na ASP.
Post a Comment