0

Vijana   wametakiwa  kuwa mstari  wa  mbele  kuzitumia  ipaavyo fursa  za  kupatiwa  mafunzo ya  ujasiriamali  ili  kujijengea  uwezo  zaidi  katika  shughuli  zao  za  kila  siku.
            

Ushauri  huo  umetolewa  na  mwenyekiti  wa  kamati  ya mifugo, utalii, uwezeshaji na habari  ya  baraza  la wawakilishi ambae  ni  mwakilishi  wa  jimbo  la  kijitoupele  Ali  Sleiman Shihata kwa nyakati tofauti alipokuwa  akizungumza  na  vijana  katika  ziara  yake  ya kutembelea  mabaraza  ya  vijana ya  wilaya za Magharibi A na B.

Amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo viongozi wanapaswa kuwa karibu na mabaraza hayo  kuanzia taifa, wilaya na shehia.

        Nae Naibu katibu mkuu uwezeshaji vijana Hassan Khatib ametoa rai kwa vijana kuwa  wabunifu na kutumia vyema fursa za mikopo wanazozipata hatua aliyoitaja kuwa itasaidia kutimiza matarajio yao katika maisha.


Miongoni mwa changamoto zilizotajwa kuyakabili mabaraza hayo katika shughuli za kiutendaji ni pamoja na ufinyu  wa  ofisi, ukosefu  wa fedha za  kuendeshea  kazi  za  mabaraza  hayo na  vitendea  kazi.

Post a Comment

 
Top