0

Katika maisha kila mmoja amejaliwa vipaji na vipawa mbalimbali ambavyo vinaweza kuwa na manufaa katika kuleta matokeo makubwa katika maisha yetu duniani na kwa wale waliotuzunguka. Ili ufanikiwe katika maisha yako ni lazima uwe tayari kuamini vitu ulivyopewa kama zawadi kutoka kwa Mungu ili kuvitumia kuleta matokeo makubwa kwa watu waliokuzunguka duniani. Hakuna mtu aliyeumbwa katika Dunia hii ili aishi kwa uoga na hofu ya kutumia vitu vizuri alivyonavyo kwa faida ya kuwasaidia wengine. 

Una kila haki na sababu ya kuheshimu ulichonacho na zaidi kuthamini ulichopewa hata kama kila mmoja hathamini hicho ulichonacho kwa sasa ila unapoamua kukithamini wewe mwenyewe binafsi ipo siku na wengine watarudi upya kwako na kukithamini. Unapaswa kufahamu wewe ni wa muhimu sana katika Dunia, na dunia inakuhitaji wewe kila wakati ili uweze kuwajibika kuleta matokeo makubwa yanayohitajika kwa muda mrefu. Kila mtu ameumbwa kwa namna ya tofauti na mwingine na lipo kusudi lililokufanya uwepo hapa duniani, hivyo hauna haja ya kuogopa kutumia zawadi ulizopewa ndani yako kuleta matokeo duniani.

Unapoogopa kuwakilisha ULICHONACHO ndani yako unakuwa unapoteza nafasi ya kusogea mbele kimaendeleo. Amua kusimamia na kuamini unachopenda kufanya ili kuleta matokeo makubwa kwa watu waliokuzunguka. Kumbuka unapoamua kutumia kipaji ulichonacho si kila mtu atakufurahia, wapo watakaoanza kukupinga ilimradi kukufanya ukate tamaa kwenye kile unachofanya. Hii ni kwa sababu kuna wapo wanaohofia utawapita kutokana umeanza kufanya kama wanachofanya wao. Amini uwezo wako pasipo kutazama ni nani anayesimama mbele yako kwa ajili ya kukupinga, endelea kufanya hadi ulete matokeo yatakayowafanya wakuthamini siku moja.

Usifiche ulichonacho kwa hofu ya kukosolewa au kupingwa na watu, bali amua kufanya unachopenda na kile moyo unachokusukuma kufanya kila siku ili kuleta matokeo makubwa kwa watu waliokuzunguka. Dunia inahitaji watu walio tayari kukubaliana na watu wanaowapinga kwani hao ndio wenye kuzalisha matokeo chanya yanayohitajika kwa watu hao hapo badae

Post a Comment

 
Top