Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Ally
Malewa(pichani) amefanya Mabadiliko ya Uongozi kwa baadhi ya Wakuu wa
Magereza Mikoa na vituo mbalimbali hapa nchini.
Mabadiliko
hayo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Katos Rugainunura amehamishiwa
Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utawala na nafasi yake inakaimiwa na
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Mzee Nyamka aliyekuwa Mkuu wa Utawala
Magereza Mkoani Morogoro.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Antonino Kilumbi aliyekuwa Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Dodoma amehamishwa kwenda Makao Makuu ya Magereza kuwa
Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Julius Sang’udi aliyekuwa Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Mbeya.
Aliyekuwa
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP
Anderson Kamtiaro anaenda kuwa Afisa Mnadhimu Magereza Mkoani Arusha na
nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Hassan
Mkwiche ambaye alikuwa ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi.
Aliyekuwa
Mkuu wa Gereza Same Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Evarist Katego
anakwenda kuwa Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP
Uwesu Ngarama amehamishiwa Makao Makuu kuwa Boharia Mkuu wa Jeshi na
nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mipango wa Jeshi ACP Athuman
Kitiku.
Aidha,
aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza
ACP Musa Kaswaka anakwenda Makao Makuu Kitengo cha Ukaguzi na nafasi
yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Ismail Mlawa
aliyekuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga. Aliyekuwa Afisa
Mdhibiti wa Fedha wa Jeshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP
Gideon Nkana anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji,
Ukonga, Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa
Magereza ACP Chacha Jakson.
Wengine
ni pamoja na aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Mbeya ACP
Kijida Mwakingi anakaimu nafasi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya,
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Abdalah Misanga anayetoka Gereza Mgumu
kwenda kuwa Mkuu wa Gereza Msalato, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP
John Itambu anayetoka Gereza Kilosa kwenda kuwa Mkuu wa Kiwanda cha
Samani Gereza Kuu Ukonga.
Kamishna
Msaidizi wa Magereza ACP Erasmus Kundy anayetoka Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Ukonga kwenda Makao Makuu Kitengo cha Habari, Kamishna
Msaidizi wa Magereza ACP Julius Ntambala aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha
Ujenzi Makao Makuu anabakia Makao Makuu Kitengo cha ujenzi kuwa Msaidizi
wa Mkuu wa Kitengo, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Sylivester Mrema
anayetoka Gereza Idete kwenda Gereza Ubena kuwa Mkuu wa Gereza.
Aliyekuwa
Mkuu wa Gereza Ubena Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Shaba Zephania
anakwenda Magereza Mkoa wa Pwani kuwa Afisa Mnadhimu, Kamishna Msaidizi
wa Magereza ACP Solomon Urio anayetoka Makao Makuu kwenda Magereza Mkoa
wa Dar es Salaam kuwa Afisa Mnadhimu pamoja na aliyekuwa Boharia Mkuu wa
Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP George
Kiria amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Uhasibu .
Mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga kuboresha utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza.
Imetolewa na:
Lucas Mboje - ASP
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza
Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara
07 Januari, 2017.
Post a Comment