Katika hatua za kutafuta Mafanikio ndani ya jambo fulani;
huwa kuna hatua inayoweza kufikia kwa mtu yoyote yule kuchoka na
kushindwa kusonga mbele na kuendelea kutafuta mafanikio halisi
anayoyahitaji. Hii ni kwa sababu ya hali halisi ya kukosa hamasiko la
kweli katika kuendelea kufanya kile kitu unachokipenda ili kukufikisha
katika Mafanikio makubwa.
Nini cha Kufanya ili kuendelea kubaki Kwenye kile kitu unachokipenda;
na zaidi pasipo kuacha au kuangalia mazingira yanayokukatisha tamaa ya
kuendelea kukifanya?
Jibu ni moja tu. Jifunze KUJIHAMASISHA Mwenyewe binafsi. Ndio. Huo ni
ukweli unaotakiwa kuujua ya kuwa; kama unahitaji kubaki katika msimamo
wako mkuu wa kusimamia jambo moja unalolifanya ili kujiletea mafanikio
makubwa ni lazima ujifunze kujihamasisha wewe mwenyewe binafsi tena kila
siku.
Unawezaje Kujihamasisha Wewe Mwenyewe Binafsi? Fuata hatua hizi 6 ili
kuhakikisha unabaki katika HAMASIKO la kweli la kuendelea kufanya kile
kitu unachokipenda.
1.) Angalia Mambo makubwa Uliyoyafanya Nyuma yako.
Hii ni njia nzuri ya kukusaidia kubaki katika kuhamasika. Jifunze
kuangalia mambo makubwa uliyoyafanya huko nyuma; angalia umewahi kufanya
mambo mangapi makubwa na kuyafanikisha; angalia jinsi ulivyoweza
kushawishi watu fulani mahali fulani kufanya jambo fulani na
wakakusikiliza. Hayo na mengine mengi yanaweza kukujengea hamasiko kubwa
la kuendelea kufanya kile kitu ulichoacha kufanya au ulichopunguza au
kuchoka kukifanya.
2.) Jenga Tabia ya Kuchukua hatua.
Usiwe mtu wa kuongea sana bali jifunze kuchukua hatua kila siku ya
kutekeleza mambo mazuri yanayoweza kukuletea mafanikio makubwa maishani
mwako. Watu hawaangalii maneno yako bali zaidi wanatafuata yale mazuri
unayoyafanya tena yanayoonekana. Hii tabia unapoijenga na kukua ndani
yako inakupa ujasiri wa kusonga mbele kutokana na yale mambo makubwa
uliyoyafanya.
3.) Simamia Jambo Moja hadi Mwisho.
Usijaribu kuwa kigeugeu kwa kupenda kufanya kila kitu; usipende
kufanya kila kitu. Watu wengi wenye kujaribu kufanya kila kitu huwa
mwisho wa siku wanaishia kushindwa, na kukata tamaa ya kuendelea kufanya
hata mambo mazuri yaliyokuwa na manufaa kwao. Jifunze kuchagua jambo
moja unaloweza kulifanya hadi mwisho ili ulifanye kwa umakini na
kulifanikisha. Kwa kufanya hivyo utakuwa unajihamasha binafsi.
4.) Acha kulalamika tena.
Usipende kulalamika bali chukua hatua na muda huo kwa kuendelea
kufanya mambo ya msingi na ambayo yana manufaa makubwa ya kukupeleka
katika safari ya mafanikio makubwa zaidi. Kulalamika kunapoteza heshima
na hatua za kusonga mbele. Chukua hatua.
5.) Endelea Kujifunza kila siku.
Usiache kujifunza kwa kusoma vitabu, kusikiliza audio books, fatilia
motivational articles and videos mbali mbali, nakadhalika. Hii ni njia
nzuri ya kukusaidia kubaki kwenye hali nzuri na hamasa kubwa ya
kufanikiwa katika kile kitu unachokipenda. Na zaidi sana unaweza
kutembelea mtandao wa www.ishindotoyako.com ili kusoma makala zitakazo kuhamasisha katika kubakia katika hatua nzuri ya kufanikiwa.
6.) Tembea na watu wenye mawazo chanya.
Huwezi kuwa miongoni mwa watu waliofanikiwa zaidi na kuendelea kubaki
katika msimamo wa kusimamia malengo na mipango yako mizuri uliyonayo
kama utaendelea kuwa katikati ya watu wenye mawazo hasi zaidi. Watu
wenye mawazo hasi mara nyingi hawatambui kile ulichonacho na kile
unachokilenga kwenye maisha yako; hawa wapo kwa ajili ya kukukatisha
tamaa ili usiendelee mbele na zaidi kukufanya kushindwa kuona hatua zako
za kufikia katika mafanikio makubwa.
Hivyo basi; unapaswa kutafuta kuwa miongoni mwa watu chanya wakati
wote. Tembea na uwe miongoni mwa watu chanya wenye kutamamani kufikia
mafanikio makubwa ya kutimiza na kufikia ndoto zao maishani. Jiunge na
klabu mbali mbali za kujisomea vitabu kama vile ya DarBookClub ambayo utapata kujifunza mambo mengi kuhusu namna ya kufanikiwa katika maisha na kufikia katika ndoto yako.
7.) Badili mazingira hasi yasiyokupa ushirikiano.
Ninaposema mazingira hasi nina maana ya mazingira yale yasiyotoa
ushirikiano kwako wewe juu ya kitu unachotaka kukifanya. Kama unaona
ofisi yako haikupi ushirikiano wa kitu unachotaka kufanya kama ndoto
katika maisha yako; unasubiri nini mahali hapo? Badili mazingira hayo.
Kama unaona bosi wako ni yupo tofauti katika kila jambo zuri
unalomwambia tafuta namna ya kubadili mazingira yako; hata kama ni kwa
kutokuondoka hapo ofisini ila ni vizuri ubadili upepo wa kutomshirikisha
tena kile kitu kizuri unachotaka kukifanya.
Wapo watu wamekosa ushirikiano wa kutosha wa kutimiza ndoto zao
kutoka kwenye familia zao; na yawezekana na familia hizo au ndugu zao
wana uwezo wa kutoa mchango wa kukufikisha mahali fulani. Usikate tamaa
na kuwasubiri tena wawe msaada zaidi kwako; bali amua kuchukua hatua na
kubadili mazingira ya kiakili na geuza moyo wako kwa kufanya mwenyewe.
Post a Comment