Rais mpya wa Ghana ataapishwa januari 6 mwaka 2017, katika taifa ambalo limetajwa na
wengine kama lenye kiwango bora zaidi cha Demokrasia Barani Afrika.
Nana Akufo-Addo, aliyekuwa wakati mmoja wakili wa haki za kibinadamu,
alimshinda kiongozi wa sasa, John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa
mwezi uliopita.
Karibu viongozi 11 wa mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo, ambako hali ya usalama tayari imeimarishwa.
Baada ya kuapishwa kwake, viongozi wa Afrika watajadiliana jinsi ya
kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia Yahya Jamme anakubali kuwa alishindwa
katika Uchaguzi Mkuu uliopita
Post a Comment