Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Magufuli, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa
Maendeleo wa Denmark Martin Bille Herman, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa
na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango.
Mhe. Herman amesema katika
mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya
Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani katika masuala
ya maendeleo ya kiuchumi.
Wakatihuohuo,
Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Mhe. Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mkapa amesema lengo
la kukutana na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Post a Comment