MFANYABIASHARA
wa ndizi amefariki dunia baada ya kupigwa na radi na wengine wanne
kujeruhiwa, wakati mvua kubwa ilioambatana na radi ikinyesha katika eneo
la Stendi kuu mjini Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Dk
Marco Mbata amemtaja Mfanyabiashara huyo kuwa ni Freman Swai mkazi wa
Mkoani Arusha, ambaye anadaiwa alikuwa Tukuyu kwaajili ya kununua
ndizi,na kwamba amefariki wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya
Makandanda baada ya kupigwa na radi ambayo pia imechana chana mti mbichi
uliokuwa karibu na kibanda ambacho marehemu alikuwa amejikinga asilowe
na mvua .
Amewataja
majeruhi kuwa ni,Oliva Ipyaja Anna Jelicho Juliana Francis Stella
Nzite, wote wakazi wa Tukuyu, ambao wametibiwa na kuruhusiwa na kwamba
mwili wa mfanyabiashara huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti cha hospitali ya makandana
Aidha
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Julius Challya amesema tayari ndugu wa
mfanyabiashara huyo wameshafahamika, lakini pia amewataka wananchi kuwa
makini matumizi ya vifaa ambavyo ni hatarishi vinavyoweza kuruhusu radi
kupiga hususani nyakati za mvua, ili kuepuka vifo visivyo vya lazima.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.