0
Ujenzi wa Mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami unaoendelea katika halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu yenye urefu wa Kilometa 4.85 kwa gharama ya Bilioni 9.192, umesababisha kukamatwa wahandisi watatu na kuwekwa rokapu baada ya kubainika mitaro yake kujengwa kwa matope .
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akiwa na kamati ya ulinzi na usalama baada ya tuhuma hizo za barabara hiyo kujengea mitaro kwa kutumia tope imemlazimu kutembelea mradi huo na kubaini ujenzi huo , ambapo alikuta kmtaro hiyo imejengwa kwa kutumia udongo huku ikichapiwa na sementi.
Kiswaga akalazimika kutumia jembe wakati wa ukaguzi huo kwa ajili ya kujiridhisha ukweli huo, ambapo pia yalitokea mabishano makubwa baina ya Mkuu huyo wa wilaya, wahandisi wa halmshauri, mhandisi mashauri kutoka NOLPLAN pamoja na Mkandarasi JASCO CO.LTD juu ya ujenzi huo kwa wanapunguza gharama.
Katika mabishano hayo yaliyodumu takribani dakika 15 wataalamu hao ambao walikuwa wakimbishia mkuu huyo wa wilaya kuwa kilichojengwa siyo mtaro bali ni mwanzo wa mtaro (foundation), huku wakikiri kuwa walitumia tope kujengea.
Kutokana na hali hiyo Kiswaga aliamuru mitaro hiyo iliyojegwa kwa tope kubomolewa mara moja, huku akiagiza kuwekwa rokapu Mkandarasi kutoka JASCO Co.Ltd, Mhandishi Mshauri NOLPLAN pamoja na Mhandisi msaidizi wa halmashauri Brayson Fadhili.

Post a Comment

 
Top