Mkuu
wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Bi Julieth Binyura, ameagiza kusakwa
na kukamatwa mara moja mganga mfawidhi wa zahanati ya Ilango katika kata
ya Kilesha, anayetuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi
milioni 24, za ujenzi wa nyumba ya mganga kwenye zahanati hiyo.
Mkuu
huyo wa wilaya ya Kalambo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ya wilaya hiyo Bi. Julieth Binyura, ametoa agizo hilo wakati
alipokuwa akiongea na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo, kwenye
kikao ambacho kimebariki kutimuliwa kazi kwa maafisa watendaji wa vijiji
kumi na nne, kwa makosa ya ubadhirifu na utoro kazini, amesema kuna
umuhimu wa mganga huyo kupatikana ili wajulikane wote waliohusika na
ubadhirifu huo.
Baadhi
ya madiwani wakiongea kwenye kikao hicho, wamekitupia lawama kitengo
cha manunuzi kwa kufanya kazi bila ya uadilifu, ikiwa ni pamoja na idara
ya ujenzi, hali inayoisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo, na
kuchangia kufanya miradi mingi kuchelewa kukamilika kwa wakati.
Post a Comment