Mmoja wa watoto wa wafalme Uarabuni amefanya jambo hilo lililozua gumzo
baada ya picha iliyosambaa mtandaoni ikionesha ndege hao wakiwa
wamewekwa sawa na abiria. Picha hii ilichapishwa katika mtandao wa
‘Reddit’ na mtu anayejiita lensoo ambapo alisema kuwa ametumiwa picha
hiyo na rafiki yake ambaye ni rubani wa ndege.
Picha hii inaonesha ndege aina ya mwewe wakiwa wamepandishwa ndege, jambo liliozua mjadala mkubwa kwenye mtandao wa Reddit
Mtu huyo alisema kwamba mwewe 80 walipandishwa ndani ya ndege wakiwa
wamefungwa mbawa zao ili wasiweze kuruka wakiwa ndani. Ingawa
haijathibitishwa bado, lakini inaaminika kuwa mwewe hawa walisafirishwa
kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar.
Shirika la Ndege la Etihad pia linaruhusu kusafirisha ndege ambapo
kwenye tovuti ya shirika hilo wameandika, Tunakubali kusafirisha mwewe
na tai ndani ya ndege kama abiria ikiwa tu nyaraka zote zinazotakiwa
zikioneshwa. Pia tunakubali ukitaka kuwasafirisha kama kifurushi cha
mzigo.
Tai ni moja ya nembo za Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo wanaruhusiwa
kuwa na hati za kusafiria (passport) kwa ajili ya ndege, hii ikiwa moja
ya mipango ya kuzuia usafirishaji haramu wa ndege hao.

Post a Comment