Mabingwa mara tatu wa kombea la Mapinduzi Simba fc
ya Dar es Salam imeanza vema mashindano ya mapinduzi Cup yanayoendelea Visiwani Zanzibar baada ya
kuwafunga goli 2-1 Timu ya Taifa Jangombe (Maarufu kama wakombozi wa Ng’ambo)
mchezo ambao umepigwa katika Uwanja wa Amani.
Mchezo huo
umepigwa majira ya saa 2:30 za Usiku
ambapo Simba walipata goli lao la kwanza kupitia kwa kiungo wake Mzamiru
Yasini katika dakika ya 28 huku Juma Luzio anaekipiga Simba kwa mkopo akitokea
Zesco United ya Zambia akifunga bao la 2 kwa Simba katika dakika ya 41, lakini Timu ya Taifa ya
Jang’ombe walipata bao la kufutia
machozi baada beki wa Simba Novatus Lufunga kujifunga katika dakika ya 76
kufuatia mpira wa kona kumgonga na kuingia wavuni
Mchezo huo ni wa kwanza kwa Simba lakini ni wa Pili
kwa Timu ya Taifa Jang’ombe baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa bao 1 kwa
sifuri dhidi ya Jang’ombe Boys mchezo ambao umepigwa siku ya ufunguzi wa mashindano hayo desember 30 katika uwanja
wa amani.
Awali majira ya saa 10:30 hapo jana, kulikuwa na
mchezo wa kwanza ambapo mabingwa watetezi URA kutoka Nchini Uganda walishuka
Dimbani kucheza na KVZ na URA kufanikiwa
kwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa 0
Kutokana na matokeo hayo katika msimamo wa kundi
A,URA yuko kileleni akiwa point 3 na magoli 2,huku Simba akiwa nafasi ya pili,
pointi zake 3 na magoli mawili na nafasi ya tatu inashikiliwa na Taifa
Jang’ombe akiwa na point 3 na goli 2 huku nafasi ya mwisho ikibakia kwa
Jang’ombe Boys ambao wamecheza mchezo 1 na kupoteza.
Ligi hiyo ya mapinduzi cup itaendelea hii leo kwa
kupigwa michezo miwili wakati mchezo wa mapema utakuwepo kati ya Zimamoto na
Azam huku mchezo wa majira ya saa mbili za Usiku ukiwakutanisha Dar es Salaam Young African dhidi ya Jamhuri
kutokea Visiwani Pemba.
Post a Comment