0

Kuna namna watu wanachanganya kuhusu vitu hivi viwili moja kipato na kingine ni maendeleo. Kuwa na maendeleo haimaanishi kuwa unakipato kikubwa sana au kuwa na kipato kidogo haimaanishi huna maendeleo au huwezi kuendelea na kufanya mambo makubwa.

Kipato ni kile kiasi unachoweza kuingiza kutokana na shuhuli Fulani unayo fanya kihalali, inaweza kuwa kwa siku, kwa saa, kwa wiki au hata kwa mwezi

Na Maendeleo ni ile hali ya kukua kutoka hali ya chini na kwenda ile ya juu, hii inaweza kuwa kiuchumi, ki elimu, ki afya au hata ki kazi na vinginevyo. Ila hapa tunatupia jicho haswaa kwenye yale maendeleo ya kichumi.

Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kufanya mtu kuendelea kiuchumi, moja wapo ikiwemo ni kipato mtu anacho weza kuingiza kutokana na shughuli anayo fanya. Hapa leo tunaongelea kipato tu cha kawaida kinavyoweza kufanya maajabu kwenye maisha yako endapo utaweza kufuata misingi kadhaa.

Mfano, Wengi bado huamini mtu kuwa na mshahara mkubwa ndio chanzo cha maendeleo, au ndio ufumbuzi wa shida na ndio namna ya kumaliza matatizo, Hapana kuna mambo mengi ya ziada yana hitajika hapa:

1.    Kupanga matumizi, usitumie tu pesa kwasababu ipo. Jua ni kiasi gani utatumia, kwa wakati gani na pia kwasababu gani. Usitumie pesa kwa mambo yasio kuwa na kipaumbele yani yale mambo yanayoweza kusubiri. Tumia kwa jinsi ulivyopanga na hakikisha hutoki nje ya mpango huo.

2.    Yape Mahitaji yako madaraja, yale ya muhimu sana yape kipaumbele na yale yasiyo ya muhimu kwa wakati ule achana nayo. Ukipanga mahitaji yako kwa mdaraja hii itakusadia kujua nini cha kuanza kutatua na kipi kitafuata. Watu wengi wanafeli kwenye kupanga matumizi kwakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja wakati kipato hakilingani na matumizi hayo na matokeo yake huishiwa wakati hakuna lililo kamilika

3.    Weka akiba, na kipato hicho kidogo unachokipata hakikisha unaweka akiba, weka sio chini ya asilia thelathini (30%) ya kila unachokipa kwa mfano umeingiza 100,000/= hakikisha unaweka 300,000/= kama akiba.

Acha nikumegee siri moja ya kutunza akiba. Nivizuri kuweka akiba lakini sio akiba tu weka akiba yenye malengo. Usipo kuwa na malengo na hicho unacho hifadhi siku moja unaweza kuja kukitumia pasipo na manufaa. Na kujikuta umepoteza muda mwingi kutunza akiba na baadae kufanya matumizi yasio ya manufaa hata kidogo.

Unapo weka akiba zingatia malengo, kwa mfano mwaka kesho nahitaji kununua kiwanja, katika manunuzi hayo natakiwa kuwa na sh million tano labda, nasema kuanzia leo nita hifadhi shilling laki nne kila mwezi hadi kufikia mwaka kesho nitakuwa nimepata pesa ya kununua kiwanja. Hayo ni malengo, lazima ujue una weka akiba kwasababu gani. Hii itakupa munkari au changamoto Zaidi ya kutafuta pesa na kutimiza lengo lako

4.    Jiepushe na mikopo isiyo na tija, Usichukue mkopo kwa mambo yanayoweza kusubiri, Chukua mkopo pale tu unapojua kiasi hicho kipo ndani ya wezo wako. usichukue mkopo ukazidi nusu ya kipato chako kwani hutaweza kullipa na kuendelea kujikimu mwisho wa siku utaendelea kukopa na kuwa na mikopo mingi isiyoweza kulipika.

5.    Usidharau pesa ndogo, Hata kama una milioni mfukoni heshimu shilingi mia iliyoko mkononi, Kwa namna hii utaendela kuwa na pesa. Pesa siku zote inampenda mtu anaye iheshimu, Pesa imekuwa na uhai siku hizi unapoitumia vibaya itapita tu mikononi mwako haitakufanyia kitu cha maana kamwe. Tazama tabia za watu wenye pesa, watu ambao huwa hawayumbi kiuchumi, wengi wao wanaijua ila hawana mazoea na pesa. Siku zote haimtoshi, haizoei na anaendelea bado kuitafuta.

Yote hapo juu ni ya muhimu kama unataka kuishi vizuri na kipato hicho kidogo unachopata. Cha muhimu ni kuwa na adabu na mipango katika matumizi na mapato yako. Inawezekana kabisa ukafanya mambo makubwa kwa mshahara huo ulionao inawezekana.

Nakutakia kila la heri kwenye Pilika za Maisha >> Stuffzoom - nafasi za kazi Tanzania

Post a Comment

 
Top