MGANGA mkuu wa Hospitali ya Wilaya Geita Rafhael Mhana pamoja na Mganga
Mfawidhi wa kituo cha Afya kata ya katoro Peter Janga wamezomewa mbele
ya Mkuu wa Wilaya hiyo Heruman Kapufi baada ya kutoa taarifa za uwongo
kuwa wananchi wote wanaochangi mfuko wa NHIF wanapata dawa zote pale
wanapokwenda kupata uduma ya Afya.
Hali hiyo imejitokeza jana majira ya saa kumi na moja jioni kwenye
mkutano wa adhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi katoro
uliokuwa na lengo la kuimiza maendeleo na kusikiliza kero za wananchi
waanza kueleza.
Mara baada ya waganga hao kumaliza kueleza juu ya upatikanaji wa dawa
ndani ya kituo chao hali ilibadilika na kuwa hivi huku wakimtaka mkuu
huyo kuwatumbua kwa kumdanganya.
Mkuu huyo wa Wilaya alilazimika kuokoa jahazi kwa kuwatuliza wananchi
hao walionekana kuwa jaziba kubwa juu ya uwongo wanaoueleza mbele ya
kiongozi huyo na hapa wakanza kueleza kero zao wanapokwenda kupata uduma
katika kituo hicho cha afya.
Walipomalizaa kutoa kero zao nyingi zilizoonekana kuwa na tija kubwa na
mkuu huyo na hapa akatoa neno juu ya wauguzi wazembe kwenye kwenye
Wilaya yake.
Mkuu huyo anaendelea na ziara yake kwenye kata 50 zilizoko ndani ya
Wilaya yake lengo likiwa ni kuimiza kuchangia maendeleo pamoja na
kusikiliza kero za wananchi.
Post a Comment